Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilfred Lwakatare
Jitihada za mawakili wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Ndg. Wilfred Lwakatare kumtoa kutoka mahabusu zimezaa matunda mchana huu baada ya Hakimu anayesikiliza kesi ya hiyo kumaliza kupitia jalada la kesi hiyo ambayo Lwakatare anatuhumiwa kwa kosa la kujaribu kumwekea sumu mhariri wa gazeti la Mwananchi Ndg. Denis Msaki. Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Aloyce Katemana alisema masharti ya dhamana hiyo ni wadhamini wawili wafanyakazi kila mmoja aweke bondi ya shilingi milioni 10 na wawe na uthibitisho wa barua na mihuri ya ofisi wanayofanyia kazi.
Hii ni habari njema kwa sana kwa Uongozi, Wanachama, Wapenzi, na Mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
No comments:
Post a Comment