Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 11, 2013

Wakenya waandamana kupinga nyongeza ya Mishahara ya Wabunge!





Kitendo cha Wabunge wa Kenya kutangaza kutaka kuongezewa mishahara kabla hata ya kuanza kuwatumikia Wananchi waliowachagua kuwawakilisha na kuwatumikia limezua Tafrani baada ya Wananchi hao kuandamana mpaka viwanja vya Bunge mjini nairobi huku wakipinga vikali hatua hiyo na kudai kwamba kama wabunge hao wanaona mshahara ni kidogo wajiuzulu na kuachia watu wengine wenye moyo wa kuwaongoza kwani tangu awali Wabunge hao walipokuwa wakiomba kura ili wachaguliwe walikuwa wakijua kiwango cha mshahara ambao wabunge wanalipwa. Kumekuwa na hisia tofautitofauti huku Wabunge wengine wakipinga nyongeza hiyo na wengine kusema wanastahili kupata nyongeza kwa kuwa sasa mishahara yao itakuwa inatozwa kodi. 

Maandamano hayo yamepangwa kuendelea kwa muda wa wiki nzima kupinga kuongezewa posho kwa wabunge. Chama kikuu cha wafanyakazi nchini Kenya COTU kinaongoza maandamano hayo kwa kushirikiana na chama cha waalimu pamoja na mashirika mengine.

Wajumbe wa Kenya ni miongoni mwa wajumbe wanaolipwa mishahara ya juu duniani. Wabunge hao wamekataa kwenda mapumzikoni wakitaka suala la mishahara lijadiliwe kwanza. Wanaoandama wanasema wanafanya hivyo kutokana na kuwa wabunge wameonyesha kutojali maslahi ya raia kwa kupitisha ripoti iliyopendekeza kuongezwa kwa mishahara yao.

No comments:

Post a Comment