Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi (Sugu)
Taarifa zilizoifikia Maisha Times muda sio mrefu zinaripoti kwamba asubuhi ya leo Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la
kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa
kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka
wa serikali.
Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa
wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani
halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina
ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno
Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na
ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.
Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo.
Mizengwe Pinda ni Mpumbavu!!!!!!
ReplyDeleteWaziri mkuu pumbaf baraza la mawazir jeee???????
ReplyDelete