Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

July 3, 2013

Kumekucha: Mbinu chafu za CCM kuvuruga uchaguzi mdogo wa Madiwani Arusha zafichuka!!!!


Naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba Kushoto na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye.

Habari za kuaminika zinasema kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameingiza nchini makontena ya Nguo-Gwanda, T-Shirts, Kofia, Kadi, Bendera za CHADEMA nk kutoka nchini China.
Mavazi sambamba na kadi hizo yatavaliwa na kutumika maalum kufanya fujo na matukio ya uvunjifu wa amani katika sehemu mbalimbali nchini haswa haswa katika uchaguzi mdogo wa Udiwani katika kata za Elerai, Themi, Kaloleni na kimandolu Manispaa ya Arusha mnamo tarehe 14/7/2013 ili kusingizia na kutengeneza mazingira kwamba vurugu hizo zimefanywa na Viongozi, Wanachama na Washabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Hizo ni baadhi ya mbinu chafu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya uratibu wa Naibu katibu mkuu wa chama hicho Mwigulu Nchemba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ili kuvuruga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mnamo tarehe 14/7/2013, mbinu ambazo tayari Viongozi wa CHADEMA wamepewa taarifa na uthibitisho kutoka kwa wasamaria wema waliomo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watakutana mapema ili kujadiliana na kutoa tamko maalum kwa vyombo vya habari na umma juu ya suala hilo.


Chanzo Jf http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/480637-mbinu-chafu-za-ccm-kuvuruga-uchaguzi-mdogo-wa-madiwani-arusha-zafichuka.html

2 comments:

  1. Anonymous11:37 AM

    TATIZO NI KWAMBA HAKUNA TAHADHARI ITAKAYOCHUKULIWA NA VYOMBO VYA DOLA KWASABABU NI HAO WASHAPEWA MAELEKEZO YA NINI CHA KUFANYA
    CHADEMA HUWA WANATOA TAARIFA MAPEMA LAKINI HAKUNA HATUA ZA DHATI ZINAZOCHUKULIWA,KATIBA INASEMA SI LAZIMA USHAHIDI ILA UKI SUSPECT UNAKAMATA

    NAFIKIRI NI WAKATI SASA WA CHADEMA KUOMBA MSAADA WA KIMATAIFA MANA UWEZEKANO WA KUTENDEWA HAKI NA VYOMBO VINAVYOHUSIKA HAPA NCHINI NI MDOGO MANA VINATUMIWA TAYARI NA RULING PARTY

    rizo de bazil

    ReplyDelete
  2. Anonymous12:47 AM

    Jeshi la polisi la ccm

    ReplyDelete