TANGAZO KWA UMMA
MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND. KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI. KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.
KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.
BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. Walipiga dili waka msakizia Lowasa ili kuficha siri kali. NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.
MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.
NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI
NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.
MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.
MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika. HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.
KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.
Tafakari chukua hatua
Chanzo: http://www.sammisago.com/2013/07/mustread-waraka-mzito-kutoka-kwa-kala.html?spref=tw&m=1
Kwisha habari yako.
ReplyDeleteNjaa inakusumbua wewe....!!!!
ReplyDelete"KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA"
ReplyDeletePumbavu na uandike waraka mwingine uwaombe msamaha raia kwa kuona shule za kata ni jambo zuri lililofanywa pamoja na matokeo unayoyaona sasa hivi. Na Nimegundua huna harakati zozote zaidi ya kujaribu kutafuta njia za kua maarufu.
Ukufa kimawazo na mtizamo, Ni Lowasa yupi hasa unayemzungumzia?
ReplyDeleteawataje kwanza walohusika kwa richmond..haya ndo maamzi magum vinginevyo ni ulaghai wa kisisa. pili awambie hayo mabilion anayohonga makanisan na miskitin yanatoka wapi? hao marafiki zake ni akina nani? wana lengo gan? akiweza hayo kwa ufasaha tutamwelewa. Umekurupuka Kala, au ndo njaa kweli
ReplyDeleteKATI YA WASANII NILIOKUWA NAWATHAMINI WEWE MMOJA WAPO !!!
ReplyDeletepumba sana huyui mshikaji na ujue na umasikini wa watanzania umechangiwa na yeye kama ni mtu wa watu mbona ye tajiri we masikini,keshakua waziri toka mzee Nyerere yupo apumzike tunataka na ambao hawajawahi kuwa madarakani wajaribu tumechoka sura za miaka mawazo yao yamechoka .
ReplyDeleteNjaa kali huyu
ReplyDeletekala hapo umechemka yeye mwenyewe kwanza awambie watanzania nani aliusika na richmond laasivyo hamna kitu! na bahati yako nzuri umeyaongea hayo baada ya tuzo lasivo usingeipata. labda nilichokiona kwako kama unamsifia kwa kujiuzuru kwakuwa watanzania hawana utamaduni wa kujiuzuru.lakini mengine shwaini
ReplyDelete"KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA"
ReplyDeleteKwa maneno haya tu Kala Jeremiah anathibitisha jinsi alivyokuwa mburula na mambo ya kijamii. Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi katu kusifia shule za kata zilizogeuka kuwa vituo vya watoto kwenda kukua kimwili badala ya kupata elimu.
Ama kweli ujinga ni mzigo na kala ameonyesha jinsi alivyo mjinga sana.
Binasfi sipo Kumhukumu mtu hapa lakini ndugu kala! Tanzania tunaipenda na hayupo alie bora kuliko Tanzania. Ninachosikitika ni kumpa mtu sifa ambazo sio zake! Kwa taarifa zako mipango mingi ya Mwanzo ilikua ni utekelezaji wa Serikali wa Awamu ya Tatu hivyo unaponiambia Maji ya Ziwa Victoria kwenda Shinyanga ni juhudi za Lowassa napata kigugumizi kidogo kwani kama unakumbuka vizuri ni Mkapa ndie aliesimama kidedea pindi Wamisri walipotaka kutushtaki umoja wa mataifa kua hatuna haki ya kutumia maji ya Ziwa Victoria kwa mnajili wa mkataba wa kikoloni!
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete