Basi la kampuni ya Mtei Express T.742 ACU linavyoonekana baada ya kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali wa kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida, kutokana na kugonga pikipiki aina ya Skygo namba T.368 BXZ na kuua abiria watatu waliokuwa kwenye pikipiki hiyo.
Diwani wa kata ya Unyambwa mkoani Singida, Shaban Satu-CCM na wenzake 11 watapanda kortini leo wakituhumiwa kuchoma moto basi la Mtei na kusababisha hasara ya Shilingi za kitanzania Milioni 70.
Siku ya Tukio
Basi hilo lilikuwa likitoka Singida kuelekea Arusha ambapo watatu wa familia moja walifariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugongwa na kuburutwa na basi la kampuni ya Mtei Express ya mjini Singida.
Watu hao ni Tamili Shaban na Kassimu wamefariki dunia papo hapo kwenye eneo la tukio ambalo ni kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida Manispaa ya Singida. Hamza amefariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Singida. Miili ya watu hao ilihifadhiwa katika chumba cha mochwari katika hospitali ya mkoa.
Baba mzazi wa watoto hao, Shaban Bunku ambaye imedaiwa ni mlinzi wa kampuni ya TTCL mjini hapa,alilazwa katika hospitali ya mkoa na hali yake ni mbaya. Inadaiwa alivunjika mguu wa kulia na damu zilikuwa zikimtoka kichwani.
“Dereva wa basi hilo alilazimika kusimamisha basi hilo kutokana na kuburuta pikipiki hiyo. Baada ya kusimamisha basi hilo wananchi wa eneo hilo walipigiana simu na ghafla walijaa na kuanza kuvunja vunja vyoo na kisha kilichoma moto”,amesema Kamwela.
No comments:
Post a Comment