Huku akisisitiza kuunga mkono UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI "UKAWA" Ndani ya bunge maalumu la katiba linalo ongozwa na wenyeviti wa vyama hivyo Dr, SLAA amesema wameamua kuunganisha nguvu nje ya bunge leo tarehe 29/03/2014 Na kuwataarifu wananchi yafuatayo>
1.Kuunganisha nguvu za kudai katiba mpya kwa wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo kuwataka wajumbe wa bunge maalumu kuwataka wafuate na kuheshimu maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba.
2.kuwa tunaunganisha nguvu kwa wadau zaidi ya vyama vya siasa kujiunga na umoja huu na kudai katiba mpya nchi nzima.
3.Kwa kuanzia tutafanya mikutano ya hadhara na ya ndani nchi nzima kushinikiza madai haya ya katiba ya wananchi.
4. Mwisho kwa kuanzia tutazindua kampeni yetu kesho tarehe 30/03/2014 jijini mwanza kwenye mkutano mkubwa wa hadahara amabao umeshaanza kutangazwa na matangazo yanaendelea mpaka muda huu.
Katibu mkuu wa NCCR amemalizia kwa kusema katiba siku zote hutungwa na wanchi waliowengi na sio watawala.
Viongozi hao wanasisitiza na kuwaomba Wananchi (Watanzania) kwa ujumla kokote walipo wajitokeze kuunga mkono kampeni hii inayoongozwa na watu wenye historia ndefu na madai ya katiba ya wananchi toka enzi za chama kimoja.
No comments:
Post a Comment