"Tumewakamata Watanzania wanne leo (jana) JKIA. Tumewaweka chini ya uangalizi na tayari wameshatoa vidonge 186 ambavyo tumevifanyia uchunguzi na kudhibitisha kuwa ni heroin," Ngisa aliliambia Shirika la Habari la Uchina kwa simu. Ameongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani leo Ijumaa.