Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

February 5, 2012

Sherehe za miaka 35 ya Chama Cha Mapinduzi zilizoazimishwa kitaifa jijini Mwanza- Watoto wa mitaani wafurika uwanja wa CCM Kirumba!



 Watoto kutoka katika kona mbalimbali za jiji la Mwanza na kufurika uwanjani hapo wakimtizama Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza kwa ustadi mkubwa Muziki wa Hakunaga uliokuwa ukitumbuizwa na Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Suma Lee.


 Rais na Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi taifa Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia Wananchi waliojitkeza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Kushoto kwake ni katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama, kulia kwake ni aliyekuwa katibu wa chama hicho mzee Yusuf Makamba na kulia kabisa ni Mke wa rais mama Salma Kikwete.

 Rais na Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi taifa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wana CCM wa jiji la Mwanza katika kuadhimisha miaka 35 ya Chama Cha Mapinduzi katika uwanja wa CCM Kirumba.



 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi hayo kutoka kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

 Rais Jakaya Kikwete punde tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.

Rais Jakaya Kikwete akikaribishwa kwa Ngoma za Asili wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza

Rais na Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi taifa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wana CCM wa jiji la Mwanza katika kuadhimisha miaka 35 ya Chama Cha Mapinduzi katika uwanja wa CCM Kirumba.

 Gwaride la Vijana wa CCM likipita kwa ukakamavu mbele ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete

 Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Suma Lee akionyesha umahiri wake alipopanda jukwaani kutumbuiza wakati wa sherehe hizo

 Mama Salma Kikwete na Spika Anne Makinda na wakinamama wakisherehekea miaka 35 ya CCM baada ya kukunwa na wimbo wa Vicky Kamata.

Wananchi wakiwa kwenye foleni kuingia katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment