Rais wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete [wa tatu nkutoka kulia] akiwa na baadhi ya Viongozi wengine wa Nchi za Afrika katika mkutano wa Uchumi uliofanyika mjini Davos,Uswisi..
Imekuwa si jambo la kushangaza kuwasikia wananchi wakiongea, kulalama, kubishana juu ya mambo mbalimbali yanayolihusu taifa likiwamo kubwa linalohusiana na safari za mara kwa mara za nje ya nchi za rais wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilihali taifa likikabiliwa na matatizo mbalimbali yenye kuhitaji usimamizi wake wa karibu kama kiongozai wa nchi mfano hili la saasa la Mgomo wa Madaktari. baadhi ya maswali ambayo Maisha Times
imekuwa ikiyasikia mara kwa mara na kuona si vibaya iwapo ikayawakilisha hadharani na kupata maoni na mchango wa pamoja kutoka kwa kila mtu ni haya yafuatayo:
1. Je Serikali ya Tanzania inaweza kuwaweka wazi wananchi wake kuhusiana na matunda yoyote ambayo yamepatikana kutokana na safari/vikao na mikutano mbalimbali ya nje ya nchi ambayo Jk amekuiwa akiihudhuria bila kukosa..??.
2. Kuna ulazima kwa rais Jk kuhudhuria kila mkutano wa nje ya nchi anaoalikwa..??..
3. Je Rais hawezi kumtuma Mwakilishi katika mikutano hiyo kama ambavyo Kenya na nchi nyingine za Afrika zinavyofanya ili japo kutoa nafasi kwake kushughulikia mambo mbalimbali yanayolikabili Taifa na yenye kuhitaji usimamizi wake wa karibu akiwa kama kiongozai wa nchi..??..
4. Watanzania wategemee nini kutokana na Safari zake hizo za tangu akiwa Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimatafa katika awamu ya tatu mpaka sasa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano-Tanzania katika awamu ya nne..??..
No comments:
Post a Comment