Mgombea wa kiti cha Urais wa Marekani kutoka chama cha Democratic, Barack Obama tayari ameshinda uchaguzi huo. Taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka vyanzo vyake nchini Marekani Obama ameshinda katika majimbo 281 kiwango ambacho mpinzani wake Mitt Romney wa chama cha Republican hawezi kukifikia tena kwa sasa.
Ingawa idadi fulani ya kura bado inahesabiwa mshindi katika kiti
hicho inatakiwa angalau ashinde katika majimbo 270, kiwango ambacho
Obama kwa sasa amekivuka hadi muda huu.
Romney hadi sasa ameambulia ushindi wa kura za majimbo 203 tu.
Kikawaida ili mgombea aweze kushinda uchaguzi wa Marekani, mgombea
anahitaji kupata angalau kura 270 katika majimbo.
No comments:
Post a Comment