Generali Gabriel Amisi
Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa
aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.
Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu,
Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa
wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia
Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo
wa majeshi, siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma
Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao pia wameuteka mji wa Sake, lakini
msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende amesema wanajeshi wa serikali
wamefanikiwa kuumboa tena mji huo mdogo.
Ikiwa rais Joseph Kabila hatakubali kuanzisha
mazungumzo ya amani waasi hao ambao inaaminika kwamba wanaungwa mkono na Serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano hayo mpaka
mji mkuu wa Kinshasa.
No comments:
Post a Comment