Watoto wengine wa vigogo wajazwa Idara ya Afya
Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, Kinondoni
Siku
chache baada ya kuibuka mjadala wa kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani
ya Benki Kuu ya Tanzania [BoT], hali kama hiyo imejitokeza tena kwenye
Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake tatu za
Temeke, Ilala na Kinondoni, Maisha Times imebaini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Idara hiyo, wametoa waraka wakihoji namna
watoto hao wa vigogo walivyoweza kushika nyadhifa kubwa katika manispaa
hizo, ilhali watumishi wengine wenye sifa, ama wakiachwa au wakipelekwa
mbali na Jiji la Dar es Salaam.
Katika
waraka huo, ambao chanzo chetu kimepata nakala yake, wanatajwa baadhi ya
watoto wa vigogo na nyadhifa zao kuwa ni Janeth George Kahama, ambaye ni
Mganga Mkuu wa Jiji. Huyu anatoka katika familia ya Mzee George Kahama,
mmoja wa mawaziri wawili walio hai wa kwanza katika Baraza la Kwanza la
Mawaziri la Tanganyika huru. Mwingine aliye hai ni Job Lusinde.
Waraka
huo pia unasema nafasi ya Mganga Mkuu Msaidizi wa Jiji la Dar es Salaam
inashikwa na Dk. Hawa Rashidi Kawawa. Huyu ni mtoto wa Mzee Rashidi
Mfaume Kawawa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Tanganyika,
Waziri Mkuu wa Tanzania, na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi [CCM].
“Hivi
ni kweli watoto hawa wa wakubwa ndiyo wenye sifa tu za kushika nyadhifa
hizi? Kweli, wanaweza kuwa na sifa, lakini iweje wasipelekwe
Tandahimba, Kibondo au Karagwe? Kwanini Dar es Salaam tu?” Wamehoji
waandishi wa waraka huo.
Wameendelea
kusema kuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ni Dk. Gunini Kate
Kamba. Huyu ni mtoto wa Kamba aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali
tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na ndani ya CCM. Wadhifa wa karibuni
kabisa aliokuwa nao ni wa ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki.
Kwa
upande wa Manispaa ya Ilala, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo ni Dk. Asha
Omar Mahita. Dk. Asha ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi [IGP] mstaafu Omar Mahita.
Mtoto
mwingine wa kigogo ni Dk. Amani Kighoma Malima ambaye ni Mganga
Mfadhiwi wa Hospitali ya Temeke. Huyu ni ndugu yake na Naibu Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Dk.
Amani ni mtoto wa marehemu Kighoma Malima, ambaye alishika nyadhifa
mbalimbali serikalini. Mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti alikuwa
Waziri wa Fedha.
Aidha,
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk. Sylvia Mamkwe, ingawa si mmoja
wa watoto wa vigogo, lakini alikuwa na uhusiano wa karibu mno wa kikazi
na aliyekuwa Mganga Watoto wengine wa vigogo wajazwa Idara ya Afya
Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, Kinondoni
Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa; aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo mwaka huu kutokana na shinikizo la madaktari waliogoma.
“Haya ni majina ya baadhi tu ya watoto wa vigogo katika Idara ya Afya
katika Jiji la Dar es Salaam na Manispaa zake. Tunauliza, iweje watoto
wa wakubwa tu ndiyo washike nyadhifa hizi kwa Dar es Salaam na si
mikoani?” Umehoji waraka huo.
Wiki
iliyopita, chanzo chetu kiliandika taarifa ya kuwapo watoto wengi wa vigogo
ndani ya BoT. Hadi sasa, majina yanayovuma ya watoto hao ni ya Pamela
Edward Lowassa, Filbert Tluway Sumaye, Zaria Rashidi Kawawa, Harriet
Matern Lumbanga, Salama Ali Hassan Mwinyi, Rachel Muganda, Salma Omar
Mahita, Justina Joseph Mungai, Kenneth Nchimbi, Blasia William Mkapa,
Violet Philemon Luhanjo, Liku Kate Kamba, Thomas Mongella na Jabir
Abdallah Kigoda.
Kuwapo kwa watoto wa wakubwa katika sehemu nyeti na nzuri kumeanza kuzua minong’ono ya upendeleo miongoni mwa wananchi.
Mmoja
wa wananchi amehoji hali hiyo kwa kusema, “Ninachojiuliza na sipati
majibu mpaka sasa ni hiki, kama imetokea coincidence [bila kutarajia]
BoT ikaajiri watoto 14 wa vigogo; je, coincidence hiyo hiyo inaweza
kutokea kwenye Wizara ya Elimu watoto wenye majina kama hayo hayo
wakapangwa kwenda kufundisha shule za kata vijijini, ambako hakuna maji
wala umeme na wakaendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo wa kizalendo bila
kujali kuwa mishahara imechelewa na hawajapandishwa vyeo; na wakati huo
huo wakiidai serikali sikivu malikimbizo?
“Hivi kweli binadamu wote ni sawa kwa maana ya fursa za ajira bila kuangaliana usoni, hasa BoT?”
No comments:
Post a Comment