Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

December 22, 2012

-§-NEMC yaifunga hotel ya "Double Tree by Hilton" kwa Uchafuzi wa mazingira!


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (katikati) akitoa amri ya kuifunga hotel ya Double Tree kutokana na kutiririsha maji taka baharini. Wa kwanza kushoto ni Bw. Karim Kanji - Mkurugenzi Mkazi wa hotel hiyo.

Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameifungia hotel ya Double Tree ya Jijini Dar es Salaam kutokana na kutiririsha maji taka baharini.
Waziri Huvisa ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Charles Kitwanga.

Ziara hiyo ililenga kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa awali na Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara kutembelea viwanda na hoteli zilizo pembezoni mwa bahari kuona mfumo wa maji taka.
Katika ziara hiyo, Hotel ya Double Tree iliagizwa kuwa na mpango wa muda mfupi na wa haraka wa kusitisha utiririshaji wa maji taka baharini ambao mpaka leo hotel hiyo ilikuwa bado haijatekeleza.
 
Sambamba na hilo na hilo Waziri Huvisa amefuta hati ya ukaguzi wa Mazingira (Environemental Audit) na kuitaka hoteli hiyo kurekebisha mara moja mfumo huo ikiwa ni sambamba na kulipa faini kwa baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Picha Zaidi za Hoteli ya  "Double Tree" 










No comments:

Post a Comment