Huyo ndiye Ben Saanane na majibu ya Zitto!
Mara ya kwanza kulisikia jina Saanane ilikuwa ni katika uchaguzi wa BAVICHA miaka kadhaa iliyopita ambapo uchaguzi huo ulimpa ushindi bwana John Heche.
Katika uchaguzi ule majina yaliyokuwa yakizungumzwa sana yalikuwa ni Ben Saanane, John Heche na Habib Mchange. Kampeni za hape na pale zilifanyika na waliokwenda kinyume na taratibu, kanuni na katiba ya CHADEMA hakika waliondolewa katika kinyang'anyiro kile na waliondolewa alikuwepo Habib Mchange aliyekutwa na kosa la kutoa rushwa kwa viongozi wa mikoa na wilaya kwa kutumia m-pesa na tigo pesa ambapo baada ya kuonyeshwa ushahidi usiyo na shaka ndani yake kutoka vodacom na tigo hakika alikubali na hatimaye kukosa sifa za kugombea.
Baada ya Mchange kuenguliwa aliweza kuwashawishi wagombea wengine akiwemo Saanane wajitoe kugombea na wamuunge mkono Mwampamba. Hakika Saanane alikubali na hatimaye wakaanza kufanya kampeni chafu dhidi ya Heche kinyume na taratibu, kanuni na katiba ya chadema kwa kufanya kampeni usiku kucha pasipo kujificha katika maeneo ya magomeni na hatimaye walipoitwa kwenye vikao halali vya chama na kuhojiwa walikiri makosa yao na hatimaye kukosa sifa za kuwa wagombea.
Baada ya hapo uchaguzi ulifanyika na hatimaye bwana John Heche aliibuka kuwa mwenyekiti wa BAVICHA.
Sintofahamu ilianza kujitokeza tokea siku hiyo ambapo wale wote waliokosa sifa za kugombea walianza kumpinga, kumchafua, kumtukana na kufanya mbinu zote za kumkwamisha bwana Heche katika majukumu yake ya kila siku pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA akiwemo mh Mbowe na Dr Slaa.
Hali hii iliendelea kwa muda mrefu kwa wasaliti hawa (masalia) kufanya vikao vya siri na kuapanga mikakati mbalimbali wakiongozwa na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa CHADEMA pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM kwa kuwapa pesa za kufanya usaliti wao akiwepo Nape Nnauye.
Baada ya nafsi kumsuta hatimaye bwana Ben Saanane aliamua kuwaambia wenzake waachane na usaliti maana haumbomoi bwana Heche bali unakibomoa pia chama na yeye hayuko tayari kuona hilo likitokea. Cha kushangaza ni kwamba wenzake hao waligoma na kuanza kumwita Saanane ni msaliti amesaliti kundi lao na wataanza kushughulikia na yeye pia.
Na kweli walianza harakati hizo za kumchafua Saanane pamoja na viongozi wa juu wa chadema na hata sms ambazo wasaliti hawa wamekuwa wakimtumia Saanane ninazo na akiniruhusu nitazileta hapa wana jamvi mzione.
Lakini baada ya kuongea na bwana Saanane aliniambia yeye ni jasiri sana na haogopi chochote na atasimamia ukweli maisha yake yote hata kama itamgharimu kifo. Nikamuuliza miongoni mwa wasaliti na waliokuwa wakiufadhili usaliti ni kina nani? Na yeye alinitajia kama ifuatavyo:-
1. Zitto Zuberi Kabwe.
2. Juliana Shonza
3. Habib Mchange.
4. Mwampamba.
5. Gwakisa
6. Nyakarungu.
Na wengine kwa sasa naomba nisiwataje kwa majina yao.
Kwa mujibu wa Saanane wasaliti hawa wameweza kuanzisha majina tofauti tofauti huku Jamii Forum na katika mitandao mingine kwa lengo la kutukana na kukashifu viongozi wa juu wa chama sana sana mh Mbowe, Dr Slaa na John Heche.
Na amenipa zaidi ya majina 20 ambayo wanayatumia vijana hawa.
Angalizo langu ni kwamba CHADEMA ni chama ambacho Watanzania walio wengi wameona ndiyo tumaini lao. Hivyo basi kwa kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu wasaliti hawa hawataweza kukidhoofisha CHADEMA maana kinasimamiwa na Mungu.
Nawasilisha.
Kujua zaidi Bofya hapa http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/370013-huyo-ndiye-ben-saanane-na-majibu-ya-zitto.html na http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/370642-juu-ya-tuhuma-kwa-zitto-na-kundi-lake-kutoka-kwa-mamuya.html
No comments:
Post a Comment