Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

December 17, 2012

-§- CNN: Dr. Slaa awa gumzo na hatari serikalini Tanzania


Habari zilizotolewa na kituo cha habari cha kimataifa cha CNN jana usiku kilikuwa na mjadala uliochukua takribani dakika 15 huku wakijikita zaidi kuhusu jinsi serikali ya Tanzania inavyoendeshwa na hatimaye wakasema kuwa kuna upinzani mkubwa sana ambao uko chini ya chama kikuu cha CHADEMA huku wakimtaja Dr Wilbrod Slaa kuwa amekuwa ni kiongozi anayetikisa viongozi wa nchi hiyo na hadi kufikia chama tawala kubadili mfumo wao wa utawala ndani ya chama tawala bila kujijua.

CNN walienda mbali zaidi na kueleza kuwa Dr Slaa ameonekana ni mtu makini na mpembuzi mkubwa wa nyaraka za wizi wa mali unaotokea nchini Tanzania.


Baada ya CNN kumaliza mjadala huo walihamia mjadala wa kujadili vifo vya watoto 20 vilivyotokea huko Marekani huku wakumuonyesha. Rais Obama akilia machozi kutokana na vifo hvyo.


Rai yangu ni kuwa hiki kituo cha CNN kitapingwa tena na CCM kuwa Dr Slaa si mtu anayewanyima usingizi kama serikali ya CCM kupitia waziri Membe alivyoamua kukipinga hiki kituo cha CNN pale kilipokuwa kinajadili mpaka wa Malawi na Tanzania?

Chanzo http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/369014-cnn-dr-slaa-awa-gumzo-na-hatari-serikalini-tanzania-18.html

3 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous3:15 PM

      Watanzania wamechachamaa hawataki ujinga wa ccm

      Delete
  2. KWA MTANZANIA MWENYE AKILI TIMAMU, HUHITAJI CNN AU BWANA NAPE NAUYE KUKUBALI KUWA DR. SLAA NI TISHIO KWA CCM..

    DR. SLAA NI MOJA YA NURU KWA WAZALENDO WACHACHE, WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI HII.

    MUNGU AMLINDE, 2015 SIO MBALI. AJICHUNGE PIA= POLITICS IS STILL A DIRTY GAME.

    ReplyDelete