Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

December 15, 2012

-§- Waraka wa moja ya mapandikizi walioko ndani ya BAVICHA wanaotajwa kumchafua na kumpinga Dr. Slaa huu hapa!

 Ndugu wanahabari rangi nyeupe katika bendera chama changu ninachokisimamia [CHADEMA] inasimamia ukweli na uwazi. ranmgi hiyo inawataka wanachadema wote kuwa wazi katika kulinda, kusimamia falsafa, itikadi na sera za chama chetu.

Nimehuzunishwa sana ka kukatishwa tama na kitendo cha undimilakuwili na umamluki wa Katibu Mkuu Bwana Slaa kwa kitendo chake cha kuendelea kumiliki kadi ya Chama cha Mapinduzi wakati akitambua kuwa yeye ni Kiongozu anyeongoza harakati za chama Kikuu cha Upinzani hivyo kutakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuonyesha mwenendo bora kwa kuishi maisha anayohubiri.
Katiba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sura ya tano ibara ya kwanza ndogo ya 5.1.6 kinachosema “Mwanachama wa CHADEMA asiwe mwanachama wa chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA” Akitambua kadi ndicho chombo kikuu kinachomtambulisha mwanachama ndani ya chama hivyo, kitendo cha kuendelea kumiliki na kulipia kadi Chama cha Mapinduzi kimedhihirisha kuwa yeye ni mbwa mwitu aliyejivika ngozi ya kondoo ndani ya upinzani.
Bwana Slaa amekuwa akiaminisha Umma kuwa yeye ni Kiongozi mzalendo safi huku akiendelea kuwatuhumu baadhi ya wanachama na viongozi wenzie kuwa ni mapandikizi,Hivyo kitendo hicho cha yeye kumiliki na kulipia ya CCM imeonyesha kuwa yuko CHADEMA kwa kazi maalum ya kuhujumu harakati za Ukombozi hivyo hana na amepoteza sifa ya kuwa Kiongozi wa Upinzani. Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ibara ya tano, BWANA WILBROAD PETER SLAA NI PANDIKIZI kutokana na sababu zifuatazo, ambazo nimejiridhisha nazo bila chembe ya shaka yoyote hivyo tunamuomba apishe uchunguzi dhidi yake ili tukiona dhamira njema tuendeleze harakati za Ukombozi yeye amepoteza sifa, kwa kitendo cha kuwa na Kadi ya chama ambacho kimetesa Watanzania na kuwanyanyasa lakini yeye bila aibu kukusanya kadi za wananchi wanaojiunga na CHADEMA kuzichoma moto na huku yeye akiwa amebaki na yake kibindoni hii imepelekea yeye kufanya kazi na umamluki na kukivuruga Chama kama ifuatavyo:-
Vilevile Bwana Slaa amekuwa akilazimisha Viongozi wa Chama Mikoani kumpokea anaedaiwa kuwa mchumb wake bibi JOSEPHINE MSHUMBISI kama Kiongozi wa chama Taifa,mchumba wake amekuwa chanzo pia cha migogoro ndani ya chama kwani amekuwa akipeleka watu majimboni na kuagiza viongozi wa Chama wamtambue kama mgombea wa ubunge mwaka 2015, Pia amekuwa akitumia rasiliamali za chama vibaya katika ziara yake.
Hii inaonyesha Bwana Slaa analipa fadhila kwa mwenyekiti huyo ambaye maamuzi yote ya baraza huamiliwa na Bwana Slaa, Mfano huu wakulipana fadhila anaoufanya Bwana Slaa ni mfumo wa CCM ambako Slaa ni mwanachama na baada ya kukiri kwamba ni kweli anamiliki Kadi ya CCM hadi leo hii.
Bwana Slaa ni Kiongozi anyejihusisha na vikundi vya majungu jambo ambalo ni kinyume na Katiba na kanuni ya Chama kwa kudhihirisha kwamba Bwana Slaa ni mamluki ndani ya CHADEMA aliyekuja kutimiza kazi maalumu amekuwa akichochea mgogoro na kuchukua maamuzi ya kuwafukuza baadhi ya vingozi ambao wamekiongoza chama kwa muda mrefu.
Bwana Slaa alifukuza viongozi wa chama Geita. Alifukuza madiwani Arusha. Hapa Mwanza alishinikiza kufukuzwa kwa madiwani wawili CHAGULANI NA MATATA bila kuzingatia falsafa ya Chama kuamini katika nguvu ya umma kwamba wananchi ambao ndio wapiga kura wenye maamuzi juu ya hao Madiwani hawakushirikishwa katika kutoa maamuzi wakati wa kuwafukuza.
Bwana Slaa amesababisha madiwani watatu kufukuzwa hapa Mwanza kwakuwakataza wasihudhurie vikao vya Halmashauri. Hivyo kwasababu kupoteza kata tatu (3) ambazo ni Ilemela, Nyamanoro na Kirumba. Kwa madai kwamba hawamtambui Meya MATATA.
Pia Bwana Slaa amekuwa akivunja uongozi wa chama bila kuzingatia Katiba ya Chama kama Geita, Nyamagana, mvomero Morogoro Lindi na Mtwara bila kufata Katiba kama inavyoeleza Ibara ya 6.3 (b) mamlaka ya nidhamu na uwajibikaji, “kwamba kingozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza kusimamishwa au kuachishwa Uongozi na Kikao kilichomteuwa”Lakini yeye amekuwa akifukuza na kuvunja Uongozi katika sehemu mbalimbali za nchi bila kuzingaita misingi ya Katiba, Anaongoza Chama kwa Mfumo wa Hailakia kwamba atakalosema yeye ndio sheria na linalotakiwa kufuatwa na haitakiwi kuhoji. Slaa amekuwa akiwafukuza na kuwaita kwa kuwatukana mamluki Vingozi ambao wamejenga Chama kwa muda mrefu bila hata ruzuku leo hii chama kinapata ruzuku ya zaidi ya Milioni 200 wanaonekana hawafai licha ya kutopelekewa ruzuku majimboni mwao.
Vilele Bwana Slaa amekuwa akilazimisha Viongozi wa Chama Mikoani kumpokea anaedaiwa kuwa mchumba wake bibi JOSEPHINE MSHUMBISI kama Kiongozi wa chama Taifa,mchumba wake amekuwa chanzo pia cha migogoro ndani ya chama kwani amekuwa akipeleka watu majimboni na kuagiza viongozi wa Chama wamtambue kama mgombea wa ubunge mwaka 2015, Pia amekuwa akitumia rasiliamali za chama vibaya katika ziara yake.
Amekuwa akichangisha michango kwa kisingizio cha M4C [vuguvugu la mabadiliko] Huku pesa hizo akizitumia kwa ajili ya taasisi yake yake binafsi iitwayo JUKWAA LA WANAWAKE kwa kifupi Josephine Mshumbusi haifahamiki kama ni mwanachama wa CHADEMA au La:- Hivyo Bwana Slaa hatuna imani nae kwani vitendo hivyo vyote vinatishia usalama wa Chama.
Jambo lingine la kusikitisha kwa wana – nyamagana na Mwanza nzima kwa ujumla bwana Slaa amemteua Ezekiel wenje mbunge wa Nyamagana kuwa mkurugenzi wa mambo ya nje makao makuu ya chama Dar es salaam hivyo wananchi wa Nyamagana hawana mbunge kwani kwa sasa anaishi Dar es salaam na kufanya kazi huko. Sasa hivi wana- nyamagana hawana tena mbunge kwani yuko Dar es salaam amekuwa mbunge wa makao Makuu.
Ndugu waandishi ,katika kudhihirisha kuwa Wenje sasa hivi sio mbunge wa wanachi bali mbunge wa Makao Makuu, Ndugu Wenje haelewi suala lolote linaloendelea jimboni kwake kwani ninyi wanahabari ni mashahidi alipotoa tamko la Uongo mbele yenu akidai machinga wa Mwanza wamesema wanampa siku 14 Mkurugenzi wa Jiji awe amejiuzuru , jambo ambalo lilithibitisha kuwa ni la uzushi kwani SHIUMA (Shirika la Umoja wa Wamachinga). Lilimjibu na kumtaka afute kauli yake kwani hajazungumza wala kuwahi kuonana na wamachinga aache kuwachonganisha na Serikali kwa manufaa yake binafsi kwani hao wameendelea kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo wakishirikiana bega begani na Mstahiki Meya na madiwani wao.
Ndugu wanahabari katika hili bwana Slaa hawezi kukwepa lawama hivyo basi kama ana uso wa aibu apishe kiti akae pembeni tujenge chama chetu.
Ndugu wanahabari:
Naamini mnakumbuka mwishoni mwa mwaka huu bwana Slaa alipokuwa anafanya ziara ya kukagua uhai wa Chama Mkoa wa Dar es saalm na majimbo yake alisikika akitekeleza na kuunga mkono mfumo kandamizi na unaofinya Demokrasia na utumiaji mbovu rasimali za nchi hii kwakuwa na wakuu wa Mkoa na Wilaya cha kustaajabisha na kushangaza bila aibu wala soni Bwana Slaa aliwataka viongozi wa Ngazi mbalimbali katika Jimbo la Kigamboni (Chadema) wawe tayari kupewa ukuu wa Wilaya na Mikoa Chadema itakapo kuchukua dola. Kitendo cha bwana Slaa kuendeleza sera za CCM kama kuwepo kwa wakuu wa Wilaya na Mikoa kinapingana moja kwa moja na sera na itikadi za CHADEMA. Kauli tata kama hii inamuhalalisha bwana Slaa kutumikia mabwana wawlili yaani CCM na CHADEMA ndio maana tunamtaka arudishe kadi ya Chadema na aendelee na Chama chake cha CCM anachotekeleza sera na itikadi zake.
Ndugu Nadhani mnakumbuka tarehe 28 /10/2012 tulikuwa na uchaguzi mdogo wa madiwani baada ya nafasi hizo kuachwa wazi kwa sababu mbalimbali. Katika uchanguzi ule CHADEMA iliambulia viti 5 (vitano) kati ya viti 29. Lakini baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa nini CHADEMA ilifanya vibaya katika uchanguzi mpaka kupelekea kupata viti vichache kiasi hiki wakati CHADEMA kwa sasa ni chama pendwa kwa Watanzania uchunguzi unaonyesha kwamba katika uchaguzi ule wa madiwani Bwana Slaa ambae alizunguka katika kata zote zilizokuwa zimeachwa wazi hakuwa na agenda ya kuhakikisha CHADEMA inashinda bali alibeba agenda yake binafsi na chama chake pendwa CCM NDIO maana Kanda ya ziwa CHADEMA tulishinda kwa asilimia 99 kwa sababu ya hujuma ya undumilakuwili Bwana Slaa.
Ndugu wanahabari:
Vyanzo vya mapato katika Vyama vya Siasa ni ruzuku kutoka Serikalini, michango mbalimbali kwa wadau, ununzi wa kadi za vyama kwa wanachama na kulipia ada ya uanachama katika vyama vyao. Bwana Slaa anakichangia CCM ili kiendelee kujiimarisha zaidi kwa kulipia ada ya uanachama . Kwa hio ujenzi na uimarishaji wa CCM unasaidiwa na uwepo wa Bwana Slaa na michango yake katika CCM.

HITIMISHO:-
Kutokana na mwenendo wa Bwana Slaa Wilbroad ninataka Mwenyekiti wa Chama Taifa achukue maamuzi sahihi ya kutuepusha na janga hili ndani ya Chama maana ni bora uwe moto au baridi kuliko kuwa vugu vugu endapo akishindwa tutaitisha maandamo nchi nzima maana Ni watanzania wazalendo wengi walioumia, kifilisika, na hata kupoteza maisha wakipigania ukombozi wa nchi hii, leo hii mamluki kama WILBROAD PETER SLAA hatuweai kukubali waturudishe nyuma katika harakati za Ukombozi. Tunamtaka ajiuzuru haraka iwezekanavyo. Hakuna kulala mpaka kieleweke.
……………………………..
MIMI SALVATORY MAGAFU
KATIBU BAVICHA MKOA WA MWANZA.


Huu ni mwendelezo wa kile ambacho kinatajwa kuwa ni mkakati maalumu wa Nape kumchafua na kumwangusha Kisiasa Dr Slaa. kujua zaidi bofya hapa http://maishatimes.blogspot.com/2012/12/kiongozi-wa-juu-bavicha-amhujumu-dr-slaa.html

2 comments:

  1. Anonymous12:46 PM

    huyo katibu wa bavicha mwanza ana matatizo,sisi kama vijana wa bavicha mkoa hatujui huo uongo anautoa wapi kama ametumwa akawaambie hatutetereki na haturudi nyuma daima mbele mpaka kieleweke m4c.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous4:30 PM

      Zitto Kabwe ni mbinafs, ndiye chanzo cha matatizo yote tuyaonayo ndani ya chadema.anathamini maslahi yake binafsi na sio chama, viongozi wenzake wala wananchi

      Delete