ALIYEKUWA AKITAPELI WATU MTANDAONI KWA JINA LA RAFIKIELIMU AJULIKANA!
Hashim Mkane, mwenye namba 0765283703 tapeli wa mtandaoni,
aliyewatapeli makumi ya wananchi kwa jina la RafikiElimu
akiwahadaa kuwapatia kazi katika taasisi mbalimbali.
Hatimaye yule tapeli sugu wa mtandaoni aliyekuwa akiwatapeli
wananchi mbalimbali kwa jina la RafikiElimu akiwahadaa kuwapatia
ajira ajulikana .
INAPOTOKA : Mnamo siku ya tarehe 11 Machi 2013, tuliripoti
kupitia blogu yetu na katika blogu mbalimbali nchini kuhusu
kuwepo kwa mtu anaye watapeli wananchi fedha kwa kutumia jina
la taasisi yetu. Tapeli huyu asiye na hata chembe ya huruma
kwa masikini wenzake, aliweka tangazo katika mtandao wa Zoom
Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi February 2013 akitangaza
nafasi za kazi z a kuvolunteer katika mikoa mbali mbali ya
Tanzania bara. Baada ya watu kutuma maombi yao, tapeli huyo
aliyekuwa akijitambulisha kwa jina bandia la EMMANUEL ALBERT na
kwamba yeye ni HR wa RafikiElimu, aliwaambia kuwa wamepata
nafasi, na kuwatumia fomu za kujaza kisha kuwataka wamtumie
shilingi elfu Tano ( Tshs. 5,000/=) za kitanzania kwa mpesa
kwenda namba 0763906931 ( AMBAYO MBAYA ZAIDI AMEISAJILI KWA
JINA LA RAFIKIELIMU)
Baada ya kumtumia pesa , tapeli huyo aliwatumia barua na
kuwaagiza kuripoti kazini katika taasisi mbalimbali, huku mmoja
kati yao akimuagiza aje kuripoti katika ofisi zetu.
Tulibaini juu ya uwepo wa utapeli huu mara baada ya
kutembelewa na mmoja kati ya wahanga wa utapeli huo. Dada
huyo aliye jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA ambaye ni
Muhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ( 2012 ) aliripoti katika
ofisi zetu siku ya tarehe 11 Machi 2013 saa nne kamili
asubuhi na kuomba kumuona HR . Baada ya kufanya naye mazungumzo
ndipo tulipo baini kuwepo kwa utapeli unao fanyika kwa jina
la taasisi yetu. Haraka haraka tukaenda kuripoti uhalifu huu
kwenye kituo kidogo cha polisi cha Chuo Kikuu Cha Dar Es
salaam, na kukabidhiwa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI KWA NJIA YA
MTANDAO.
Mara baada ya kupata RB moja kwa moja tulipost taarifa ya
kuwatahadharisha wananchi juu ya uwepo wa mtu anaye tapeli
watu kwa kutumia jina la taasisi yetu, huku tukiwaachia polisi
na kazi ya uchunguzi wa tukio hili la uhalifu. Wakati polisi
wakiwa bado wanaendelea na uchunguzi, siku ya Jumatatu ya
jana, tarehe 11 Machi 2013 saa sita kamili asubuhi, tulipokea
simu kutoka kwa mwakilishi wetu wa Mwanza, Dada HADIJA SEJA
akiomba tumpe namba za " MR. EMMANUEL ALBERT " ( HR wa
RafikiElimu Foundation ).. Kwa kuwa tayari tulikuwa na taarifa
za jina hilo, tulimuomba dada Hadija Seja atutaarifu kitu gani
kimetokea. Dada Hadija alitupa taarifa ya kusikitisha sana,
kwamba kuna mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja tu la Gerlad
kutoka Arusha, amewasili jijini Mwanza kuripoti katika ofisi za
taasisi ya RESTLESS DEVELOPMENT kwa ajili ya kuanza kazi. Mtu
huyo naye ni muhanga wa tapeli huyu, na baada ya kumtumia
tapeli huyo sh. elfu tano, tapeli alimuagiza aende kuripoti
jijini Mwanza katika ofisi za RESTLESS DEVELOPMENT (mabazo
kimsingi hazipo Mwanza) Can You imagine, huu ni unyama wa
kiwango gani, kumfanyia masikini mwenzako ushenzi kama huo?
Baada ya kupata taarifa hii, moja kwa moja tukaamua sisi
wenyewe kama taasisi kwenda katika ofisi za VODACOM makao
makuu zilizopo Mlimani City ili kuweza kumbaini mtu anaye
fanya unyama huu
Tunashukuru sana Mungu, Vodacom walitupa ushirikiano wa kutosha..
Kutoka kwenye database za Vodacom, tuligundua kwamba, mtumiaji
wa 0763906931 anaishi Njombe. Namba hii imesajiliwa MPESA
tarehe 02 February 2013, hakusajili kwa kitambulisho chake
halisi, bali kwa barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za
Mitaa. Alisajili akiwa NJOMBE na alipokea simu nyingi sana.
Zaidi ya watu kumi waliingia katika mkenge wake na kumtumia
hizo shilingi Elfu Tano.
Mwanzoni alikuwa ana toa hela zake kwa wakala ambaye alisajilia
namba hii, lakini baadaye alisafiri na kwenda tarafa nyingine
hivyo basi kushindwa kutoa hela kwa sababu namba ameisajili
kwa jina ambalo sio lake. Hivyo basi ili kuweza kutoa pesa
ilimbidi, ajihamishie salio kutoka katika namba 076390631 kwenda
kwenye namba yake halisi ambayo ni 0765283703. Hapo ndipo
tulipo weza kumbaini tapeli huyu.
Jina la huyu mtu anaitwa
HASHIM MKANE na namba yake halisi ni 0765283703.
Ni mkaazi wa Njombe na amehitimu Chuo Kikuu Cha Sokoine (SUA) . Aliwahi kuomba nafasi ya uwakala wa RafikiElimu katika
wilaya ya Njombe, mwezi Agosti 2012.
Baada ya kupata taarifa hizi tuliamua kutafuta mbinu za
kumkamata kirahisi,ambapo tulimtumia barua pepe, jana jioni kisha
ujumbe mfupi wa maneno (SMS) tukimwambia aje Dar Es salaam
kuhudhuria semina ya siku tano ya mawakala wa RafikiElimu (Tukamtajia na malipo) Nadhani alistukia kwamba huenda
ameshajulikana, akatuma ujumbe mfupi wa maneno uliosomeka :
" Nashukuru kwa taarifa hii ingawa nitashindwa
kuhudhuria kwa kuwa taarifa imechelewa kufika na ukichukulia
mimi ni mwajiliwa wa taasisi binafsi hivyo kuweza kupata
ruhusa kwa siku moja au mbili ilihali tunafanya evaluation
ya mradi ni ngumu. natumai kuhudhuria semina nyingine kama
mtaiandaa "
Hapa tukajua jamaa ameshastukia mchezo na uwezekano wa
kumkamata kwa njia hiyo usingekuwa rahisi. Hivyo basi tumeamua
kuweka taarifa hii mtandaoni pamoja na picha za mtuhumiwa
huyu, ili kwa yoyote yule atakaye fanikisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyu aweze kupewa zawadi nono ya shilingi Laki Tano
za kitanzania . Taarifa nyingine zitatumwa kwenye magazeti na
televisheni ili iwe rahisi kusambaza ujumbe kwa watanzania
wengi na hivyo kurahisisha kutiwa hatiani kwa dhalimu huyu .
Tafadhali upatapo ujumbe huu, wafahamishe na ndugu jamaa na
marafiki zako woote...
UKIMUONA MTU HUYU, TOA TAARIFA KATIKA KITUO CHOCHOTE CHA POLISI
KILICHO KARIBU NAWE , KISHA WASILIANA NASI KWA SIMU 0782405936.
NA ENDAPO TAARIFA YAKO ITASAIDIA KUKAMATWA KWA TAPELI HUYU,
TUTAKUPATIA ZAWADI YA FEDHA TASLIMU ZA KITANZANIA SHILINGI
LAKI TANO ( Tsh. 500,000/ =)..
Huyu jamaa ni mpumbavu...njaa na ujinga wake eti anatapeli buku tano 5 sass zitampeleka wapi??hata mimi niliapply hiyo post kumbe nimeapply ya mpuuzi niliyegraduate nae....mwaka mmoja......mxxxxuuuuu!!
ReplyDelete