Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

May 22, 2013

BREAKING NEWS: Kutoka Mtwara Part 2

Kwa sasa Wananchi wa Mtwara wamevamia eneo la viwanda ambalo lilikuwa limetengwa maalum kwaajili ya wawekezaji wa nishati ya Gesi na kuchoma moto vifaa na mitambo mbalimbali vya gharama ambayo haijaweza kujulikana mara moja. 

Mpaka sasa hivi raia wa kigeni "wazungu" kadhaa waliokuwa wakiendelea na shughuli mbalimbali katika bandari ya mtwara wameonekana wakiondoka, ni msafara wa magari yasiyopungua 25.

Barabara ya Dar-Mtwara yafungwa, Mabasi ya Dar-Mtwara yameishia Lindi

Askari 4 wa JWTZ wakiwa miongoni mwa askari 32 hivi kutoka kambi ya Nachingwea wamefariki katika ajali ya gari wakielekea mjini Mtwara kukipa nguvu kikosi cha FFU ambaco kimeonekana kuzidiwa na vurugu za wananchi wanaopinga boma la gesi kujengwa.

Kujua mengi ya zaidi endelea kufuatilia maishatimes.blogsport.com

Hotuba ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Wizara ya Nishati na madini-John Mnyika (Mb) Kuhusu Maoni ya kambi rasmi ya Upinzani juu ya mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/2014 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Bofya Hapa
 http://mnyika.blogspot.com/2013/05/hotuba-ya-msemaji-wa-kambi-rasmi-ya.html

No comments:

Post a Comment