Mzee Nelson Madiba Mandela
Habari zilizoifikia maisha Times Blog muda mchache uliopita zinaripoti kwamba hali ya kiafya ya Mpigania ukombozi na aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Madiba Mandela mwenye umri wa miaka 94 imeendelea kuwa tete akisumbuliwa na maradhi ya mapafu na kulazimu kulazwa katika Hospital moja iliyoko jijini Pretoria afrika ya Kusini, kwa taarifa za awali za madaktari zinasema kwamba maradhi hayo ya mapafu yanayomsumbua mzee Mandela yalisababishwa na mazingira sambamba na kazi ngumu alizokuwa akizifanya kipindi alipokuwa amefungwa Gerezani. Habari zaidi zinasema kwamba Mzee Mandela alifikishwa hospitalini hapo baada ya hali yake kuwa mbaya usiku wa kuamkia leo.
Kwa habari zaidi kuhusu hali ya Mzee Nelson Madiba Mandela Bofya Hapa http://www.independent.co.uk/news/world/africa/nelson-mandela-back-in-hospital-with-serious-lung-infection-8650531.html
No comments:
Post a Comment