Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

January 28, 2014

Wafuasi wa CHADEMA Mbeya: Mkuki kwa wengine "Mtamu" kwa Zitto "Mchungu"!

 Hii ni wakati Zitto Kabwe akiingia mkoani Kigoma na hawa ni baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA mkoani Kigoma wakichoma ubani kwenye jeneza lililokuwa na ujumbe kwa chama na viongozi wa CHADEMA, jambo ambalo Zitto Kabwe aliliona na kutolikemea!

Zitto Kabwe akuhutubia mkoani Kigoma katika Mkutano wake alioufanya miezi kadhaa iliyopita

Wafuasi wa CHADEMA jijini Mbeya wakiwa wamebeba mfano wa jeneza kama majibu ya kile  Chama na Viongozi wa CHADEMA walichofanyiwa na wafuasi wa Zitto mkoani Kigoma! 

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Ruanda, Nzovwe jijini Mbeya jijini Mbeya siku chache zilizopita.

Hii ni status ya Zitto kabwe katika ukurasa wake wa Facebook: "Chuki za kisiasa za kiwango hiki ni hatari sana. Viongozi wakuu kutokukemea mambo kama haya ni ishara ya udhaifu na kukosa busara. Kamwe sitalipa ubaya. Wema kwa ubaya ndio silaha tosha na mungu siku zote yupo na wanyonge. Nimechukizwa. Mola atawasamehe maana hawajui watendalo".

Hata hivyo Dr Slaa na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini walikemea kitendo hicho cha wafuasi hao kubeba mfano wa jeneza hilo lililokuwa na maandishi yaliyokuwa yameandikwa "Buriani Zitto" nk, na kusema kwamba kinaweza kupelekea chuki na kutoelewana.

Maisha Times ilipowahoji baadhi ya wafuasi walioonyeshwa kufurahishwa na kitendo hicho walijibu na kusema namnukuu "lengo letu sio baya bali tunataka kufikisha ujumbe kwa Zitto Kabwe kwamba amekufa Kisiasa na sio vinginevyo kama wengi wanavyoweza kufikiria" 

Maandishi makubwa hapo chini ni mmoja wa Wafuasi wa CHADEMA aliyeamua kufunguka kuhusiana na Status ya Zitto Kabwe katika Ukurasa wake wa facebook iliyokuwa ikiwalaumu Viongozi wa CHADEMA kuhusiana na kile kilichotokea katika viwanja vya Ruanda, Nzovwe jijini Mbeya wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilboad Slaa

"ETI ZITTO AMSIKITISHWA NA KUKASILIKA KWA KITENDO CHA WANACHADEMA WA MBEYA KUMTENGENEZEA JENEZA LINALOMUONYESHA AMEKUFA KISIASA.

ZITTO AMEKEMEA KITENDO HICHI NA KUWA HATENDEWI HAKI NA WANANCHI HAWA WALIOFANYA KITENDO HIKI.

NAMSHANGAA HUYU Zitto Kabwe KWA KULALAMIKA KUWA HAJATENDEWA HAKI NA WANACHADEMA WA MBEYA KWA KUMDHALILISHA KWENYE MABANGO NA KUMCHONGEA JENEZA,MBONA ZITTO MWENYEWE HAKUWAKEMEA VIJANA WAKE WALIOKUWA WAMEONYESHA MABANGO YA MATUSI NA KUVURUGA BAADHI YA MIKUTANO KWENYE ZIARA YA DR.SLAA NA PIA KAMA UNAVYOONA PICHA NYINGINE AMBAYO ILIKUWA INAONYESHA JENEZA LA DR.SLAA LIKICHOMEWA UBANI MKOANI WA KIGOMA MWEZI DECEMBER?ANALAUMU KWAMBA VIONGOZI WA CHAMA WAMESHINDWA KUWAKEMEA WATU HAWA WALIOMTENGENEZEA JENEZA MKOANI MBEYA, MBONA YEYE HAKUWAKEMEA WALIOKUJA NA MABANGO YA MATUSI KWENYE MIKUTANO YA CHADEMA ILIYOKUWA INAONGOZWA NA DR.SLAA MKOANI KIGOMA?ZAIDI ALICHOKIFANYA NI KWENDA KUFANYA MIKUTANO YA KUWAPONGEZA BAADA TU YA DR.SLAA KUONDOKA.DR.SLAA ALIWEKEWA JENEZA NA KUCHOMA UBANI ZITTO ALIKAA KIMYA LEO ANALALAMIKA WATU WA MBEYA KWA KUMCHONGEA JENEZA HUYU NI MTU WA AINA GANI?

NIA YA SHETANI NI KUHAKIKISHA WATU WANAMUASI MUNGU ILI WAWE WATUMWA WA ZAMBI WAKUMBWE NA SHIDA NA DHIKI MBALIMBALI NA NDO MPANGO WA ZITTO KWA KUWA AMELIPWA BILION 3.6 ILI AIVURUGE CHADEMA WATANZANIA WASIPATE NEEMA WAENDELEE KUWA WATUMWA KWENYE UTAWALA WA CCM.

KWA KUWA CCM INA UKIMWI ZITTO ANATUMIKA KAMA DAWA YA KUONGEZA SIKU ZA CCM YANI ARV LAKINI LAZIMA CCM IFE TU.

KAMA YEYE NI MZALENDO NA MPENDA HAKI ANGEANZA KUKEMEA VITENDO HIVYO KIGOMA KWENYE ZIARA YA DR.SLAA HAPA AMECHEMKA AJIPANGE, AU MGANGA WAKE WA JADI KULE SUMBAWANGA ALIKOPIGA KAMBI SIKU KADHAA NDIYE ALIYEMUAMBIA AONGEE UPUUZI HUU. AMECHEMSHA KABISA NA HAWEZI KUFANIKIWA"


Mdude Chadema Nyagali

No comments:

Post a Comment