Rais wa Misri Mohammed Mosri anaendelea kukabiliwa na
shinikizo kali huku maafisa zaidi wa serikali yake wakiendelea
kujiuzulu nao waandamanaji wakianza kukusanyika tena katika bustani ya
Tahrir.
Msemaji wa rais na mwenzake wa baraza la
mawaziri nao pia wamejiuzulu , baada ya mawaziri sita kuondoka serikali
mwishoni mwa wiki kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali.Chama rasmi cha upinzani National Salvation Front, kimesema kinaunga mkono tamko la jeshi lakini katu hakiungi mkono mapinduzi ya kijeshi.
Taarifa hiyo ya rais imesema kuwa hatua hiyo ya jeshi kuingilia kati itazua hali ya suitofahamu zaidi.
Jeshi limekanusha madai kuwa makataa hayo ni sawa mapinduzi ya kijeshi.
Serikali imesema kuwa Morsi amewasiliana na rais Barack Obama kuhusu hali ya kisiasa inayoshuhudiwa Misri.
Wakati huohuo, shirika la habari la kitaifa Misri, limeripoti kuwa waziri wa mambo ya nje Mohamed Kamel Amr amejiuzulu.
Ikiwa ombi lake litakubaliwa, atakuwa mmoja wa mawaziri wengine watano ambao wamejiuzulu kufuatia mgogoro huo wa kisiasa.
Mnamo jumapili, mamilioni walifanya maandamano wakimtaka rais ajiuzulu.
Maandamano mengine makubwa yalishuhudiwa Jumatatu na kuendelea mpaka siku ya leo (Alhamisi) huku ripoti zikisema kuwa watu wanane waliuawa wakati waandamanaji walipovamia makao makuu ya chama tawala cha Muslim Brotherhood.
Wapinzani wa Morsi, wanamkosoa kwa kuweka maslahi ya chama mbele huku akiwapuuza wale wasiounga chama hicho.
Morsi alichaguliwa kama rais wa kwanza wa kiisilamu katika uchaguzi wa mwezi Juni mwaka 2012 tarehe 30 baada ya kushinda uchaguzi uliotazamiwa na wengi kuwa huru na wa haki baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani Hosni Mubarak.
No comments:
Post a Comment