MIFANO YA KESI ZILIZOHUKUMIWA KULINDA MAKUNDI YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA
Habari hii inatokana na hatua ya Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya (CCM) aliyesukuma mashambulizi mazito na akiwatuhumu baadhi ya majaji wa Mahakama Kuu, watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na Idara ya Mahakama kwa madai ya kushirikiana na wauzaji wa dawa za kulevya, ilizua mshituko mkubwa miongoni mwa jamii.
Katika hoja yake binafsi bungeni mnamo tarehe 04/11/2013 Bulaya alisema baadhi ya watumishi katika ofisi hizo wamekuwa wakishirikiana na watu wanaokamatwa na dawa za kulevya kwa kuwapa siri na mbinu za kuharibu ushahidi ili washinde kesi.
Bulaya alisema: “Kutokana na kupanuka kwa mtandao huu wa kuhujumu, licha ya kushirikiana na washitakiwa, mtandao uliopo katika ofisi hiyo ya DPP umekuwa ukituhumiwa kufanya njama za kushirikiana na baadhi ya watumishi wa mahakama, hasa majaji kuhamisha kesi kupeleka kwa majaji ambao wanadaiwa kuhusika na mtandao huu.”
Wadadisi wa mambo wamedai kuwa hatua ya Bulaya ni ya ujasiri na ameyaweka rehani maisha yake kutokana na uzito wa suala hilo ambalo limekuwa likiitesa serikali kwa muda mrefu.
Wamedai kuwa mbunge huyo ameonyesha ujasiri wa hali ya juu, na kwamba kwa kila namna amewatisha vigogo wanaodaiwa kuhusika na biashara hiyo, hivyo kama asipolindwa na serikali maisha yake huenda yakawa hatarini.
Hofu ya wadadisi wa mambo inatokana na ukweli kwamba, mbunge mwingine kijana wa CCM, Amina Chifupa, aliyekufa miezi michache tu baadaye baada ya kuchachamaa bungeni akiitaka serikali kutaja majina ya wauza ‘unga’ hadharani, huku yeye mwenyewe akiweka bayana kuwa yuko tayari kumtaja hata mumewe, Mohamed Mpakanjia, ikiwa atagundua kuwa anafanya biashara hiyo.
Katika kesi ya Mwinyi Rashid Ismail Mkoko (KLR /IR 4143/2011), mshitakiwa aliomba dhamana Mahakama Kuu wakati kesi ilikuwa bado ipo Mahakama ya Kisutu ndipo wakili wa serikali akamwambia Jaji kuwa anaomba kuifuta.Alisema Jaji huku akifahamu kuwa kesi hiyo imefika mbele yake kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana tu, na kuwa ilikuwa haijafikishwa Mahakama Kuu kwa utaratibu wa sheria, aliamua kumfutia kesi mshitakiwa na kuamuru kuwa yuko huru.
Katika kesi Na. 794/2011 katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, hakimu aliwafunga kifungo cha nje kwa miezi 15 washitakiwa, Abdulrahman Shaban Sindanema, Said Nassoro Khamis na Abdulrahim Haroub Said waliokiri kosa la kuuza na kusambaza dawa za kulevya aina ya heroin.
Kwa mujibu wa Bulaya adhabu iliyotolewa na hakimu huyu, haipo kwa mujibu wa sheria kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya kuzuia dawa za kulevya, adhabu iliyowekwa kwa wauzaji au wasambazaji wa dawa za kulevya ni kifungo cha maisha na si chini ya miaka ishirini jela kwa kipindi hicho.
Alitoa mfano wa kesi nyingine kuwa ni Na. 274/2005, Jamhuri dhidi ya Yusuph Hashim Nyose, aliyekamatwa na kilo 1.3 za dawa za kulevya aina ya heroin alizokuwa amemeza na kisha kuzitoa kupitia njia ya haja kubwa baada ya kukamatwa na zilikuwa na thamani ya shilingi 12,600,000.
Pamoja na ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi sita wa upande wa Jamhuri, ikiwa ni pamoja na mkemia aliyethibitisha kuwa ni dawa za kulevya na mashahidi walioshuhudia mshitakiwa akizitoa kwa njia ya haja kubwa, hakimu alimwachilia huru.
Kwa kipindi cha miaka mitatu tu (2010-2013), wakati tani 64 za dawa za kulevya zilipita bila kukamatwa…zikiwa mtaani zikiharibu vijana na watoto wetu, katika kipindi hicho hicho kiasi kilichoweza kukamatwa ni tani 1.6 tu!
Takwimu hizo za kutisha zinatoa picha kwamba sehemu kubwa ya shehena za dawa za kulevya hupitishwa bila kugundulika au kukamatwa na vyombo vya dola.”
Mtoa mada alishangaa kwamba ni kwa bahati mbaya, licha ya ukubwa wa tatizo, pamoja na athari zake kwa jamii ya Watanzania, hakuna tafiti zinazoonyesha ukubwa wa tatizo kwa nchi nzima, huku vyombo vya dola vikiwa ndivyo vinara wa kuwatorosha watuhumiwa wanaoendesha biashara hii, ikiwemo ofisi ya DPP na Idara ya Mahakama.
Baada ya mbunge huyo kueleza kwa kina mambo ambayo yanabainisha na kuweka shaka juu ya uadilifu na uaminifu wa watoa haki katika mahakama zetu na ofisi ya DPP na vyombo vya usalama, Sendeka alitaka serikali itoe majibu kuhusu suala hilo la vita dhidi ya dawa za kulevya ambalo si jukumu la Mahakama na vyombo vya usalama pekee bali Tanzania kwa ujumla.
Alibainisha kuwa ili wananchi waweze kujua jinsi waliotoa uamuzi au hukumu ambayo haikuwa kwenye misingi, sheria na mahakama zilivyochukua hatua dhidi ya mahakimu na majaji walio husika.
Mara baada ya Sendeka kumaliza kuomba mwongozo huo, Naibu Spika, Job Ndugai, alitoa fursa kwa Waziri Lukuvi, ambaye alisema serikali inaandaa taarifa inayoeleza jitihada za serikali. “Serikali imejiandaa kutoa kauli kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria na itatoka kabla ya kuondoka hapa bungeni, na itaeleza tulivyojipanga kuunda chombo kipya cha kushughulikia.
Chini ni vyanzo mbalimbali vinavyohusiana na matukio mbalimbali ya Madawa ya Kulevya nchini Tanzania
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Mnigeria-wa-dawa-za-kulevya-hakupita-Tanzania-/-/1597296/1998514/-/1365vslz/-/index.html
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/mume-wa-jack-patrick-anaswa
http://www.ippmedia.com/frontend/?l=59073
http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1992390/-/x98hm2/-/index.html
http://www.freemedia.co.tz/daima/ester-bulaya-ajilipua/
No comments:
Post a Comment