Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

March 4, 2014

Mwenyekiti wa Chama cha "ACT" pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha "ADC"!


 Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) Lucas Kadawi Limbu.

 Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT Ndg. Lucas Kadawi Limbu (kushoto) na Samsoni Mwigamba (Kulia)

Imefahamika kwamba Mwenyekiti wa Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT) ngazi ya taifa pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha siasa Alliance For Democratic Change (ADC) Lucas Kadawi Limbu! 

Hali hiyo imezidi kuwachanganya wengi ambao wamekuwa wakifuatilia duru za siasa za Tanzania na kuziita "Siasa za maji taka" kutokana na wengi kukaririwa wakisema kwamba kuibuka kwa vyama vingi vidogo vidogo kunakoendelea kila kukicha ambavyo havina impact yoyote kwa Serikali iliyoko madarakani wala wananchi ni kwaajili ya maslahi ya watu wachache wanaothamini matumbo yao zaidi kunaweza kuchukuliwa kwamba ni namna nyingine ya utapeli wa kisiasa kama ambavyo Mwenyekiti wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) Ndg. Lucas Kadawi Limbu alivyoweza kumiliki kadi za vyama viwili (ADC & ACT) kwa wakati mmoja, upande mmoja akiwa ni Mwenyekiti wa chama cha ACT ngazi ya taifa huku kwa upande wa pili akibakia katika nafasi yake ya awali ya Ukatibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC).

Maisha Times ilipojaribu kuhoji kwa undani dhidi ya kitendo cha Ndg. Lucas Kadawi Limbu kuwa na sura mbili katika vyama viwili tofauti vya siasa wengi walisema kwamba wanamuona kama ni mtu asiye na msimamo na tapeli wa kisiasa na kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa vilivyoingia kwenye ulingo wa siasa za Tanzania kwa fujo na kufa kibudu kama UDP, CCJ, CHAUMA, TLP nk ndivyo itakavyokuwa kwa ACT ambacho kinadaiwa kuundwa na viongozi na wanachama walioasi, kusaliti na kufukuzwa katika vyama vingine vya siasa nchini!

No comments:

Post a Comment